Jinsi ya kupiga gari la wagonjwa kwa kiswahili

Video hii itakuonyesha wakati na jinsi ya kuita ambulensi na nini kitatokea wakati ambulensi inakuja. Pia inaonyesha jinsi ya kupata mkalimani ikiwa unazungumza lugha nyingine isiyokuwa Kiingereza.

Duration 5:29 |

Habari! Video hii itakuonyesha jinsi ya kupigia ambulensi wakati wa dharura.

Piga Sufuri Mara Tatu (000) kuita ambulensi ikiwa wewe au mtu mwingine ni mgonjwa sana, au mtu amejeruhiwa katika ajali.

Unaweza kuomba mkalimani bila malipo.

Ikiwa huna uhakika, pigia simu ambulensi.

Unapaswa kupigia simu ambulensi ikiwa una:

  • maumivu ya kifua au kubanwa
  • udhaifu wa ghafla katika uso, mkono au mguu au shida ya kuzungumza
  • kutokwa na damu ambayo haisimami
  • shida kupumua
  • kuzimia au kuanguka ghafla
  • mshtuko au kifafa
  • kuungua sana
  • au ikiwa mtu ameumizwa katika ajali ya gari au kimwili na mtu mwingine.

Unapaswa kupigia simu ambulensi ikiwa mtoto wako:

  • anakuwa mgonjwa haraka
  • ana shida kupumua
  • ana rangi au bluu kuzunguka midomo
  • anashikwa na usingizi au haitikii sauti yako
  • ana mshtuko au kifafa
  • ana ajali mbaya au jeraha kama vile mfupa uliovunjika au kukatwa kwa kina.

Unapopiga Sifuri Mara Tatu (000), opereta atauliza ‘Police, Fire or Ambulance?’. Unahitaji kusema ‘Ambulance’.

Halafu atakuuliza ‘Suburb and State’’. Unaweza kusema kitongoji kama ‘Townsville’, and Queensland.

Unaweza kuuliza opereta kwa mkalimani bila malipo kwa kusema: ‘I need an interpreter in Swahili.’

Huenda itachukua muda kukupatia mkalimani, kwa hivyo jaribu kumwambia anwani yako kwa Kiingereza ikiwa unaweza na ubaki kwenye simu.

Wakati mwingine wanaweza kutuma ambulensi mara moja.

Unahitaji kutoa habari hii wakati anapouliza:

  • Uko mahali gani
  • Nambari yako ya simu na jina
  • Eleza dharura:
    • Nini kilitokea?
    • Ni watu wangapi wameumia au wagonjwa?
    • Je, uko na mtu huyo?
    • Je, mgonjwa ana umri gani?
    • Je, ameamka?
    • Je, anapumua?

Mkalimani atamwambia opereta taarifa zako na kisha kutuma ambulensi ikihitajika.

Ambulensi ni bure katika Queensland.

Unaposubiri ambulensi, huenda ukahitaji kukaa kwenye simu hadi ambulensi ifike.

Mkalimani anaweza kukuambia njia za kumsaidia mgonjwa au aliyejeruhiwa.

Wakati unaposubiri ambulensi, kaa na mgonjwa au mtu aliyejeruhiwa.

Ukiweza, tafuta kadi ya Medicare ya mgonjwa (ikiwa anayo), kadi ya huduma ya afya, maelezo ya bima ya afya ya kibinafsi, dawa za matibabu na maelezo ya daktari wake.

Ikiwa bado uko kwenye simu, mwambie mkalimani kwamba ambulensi imefika.

Wahudumu wa afya watamhudumia mgonjwa.

Mkalimani kwenye simu atakuambia wakati wa kukata simu.

Unaweza kuuliza wahudumu wa afya ukaenda kwenye gari la wagonjwa pamoja na mgonjwa hospitalini.

Unaweza pia kuomba mkalimani katika ambulensi na hospitalini bila malipo.

Siku chache au wiki baadaye…

Kumbuka kuweka miadi ya kufuatilia na daktari wako baada ya dharura.

Ikiwa sio dharura lakini unahitaji ushauri wa kiafya, piga simu 13 HEALTH kwenye 13 43 25 84 kuzungumza na nesi. Anaweza kupata mkalimani kwenye simu kwa ajili yako bila malipo.